Tuesday, March 19

”Alikiba Anatumia Uwezo Wake kutupanga”-Abdukiba

0


''Alikiba anatumia uwezo wake kutupanga''-Abdukiba

¬† Wasanii waliopo chini ya Label ya Kings Music inayomilikiwa na msanii Alikiba, wamefunguka kuwa ‘boss’ wao huyo ndio mtu anayewafundisha vitu vingi kuhusu muziki ikiwemo mpangilio wa nani aanze kwenye ngoma zao.

Abdukiba amefunguka hayo leo kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio, wakati wanatambulisha ngoma yao mpya ‘Toto’ ambapo amekiri kuwa kwa ukongwe wa Alikiba kwenye muziki lazima awaongoze.

”Anayetupanga ni Alikiba yeye anajua vitu vingi kwenye muziki na ndio maana ana nafasi hiyo ya kushauri nani aanza na nani anafuata na nani atamaliza, kwahiyo Kings Music ni chuo cha muziki”, amesema Abdukiba.

Naye mmoja wa wasanii wa Label hiyo Killy amesema tayari kwa nyimbo mbili ambazo wamezitoa ikiwemo Sina, zimeshawaletea mashabiki wa aina mbalimbali na majina yameanza kuwa makubwa.

Abdukiba pia amesema kitendo cha Alikiba kutoimba kwenye ‘Toto’ ni sehemu tu ya mambo mazuri ambayo yapo ndani ya Kings Music na kinachofuata huenda yeye akakosekana au kila msanii akatoa ngoma yake. Wasanii wa Kings Music ni Abdukiba, Cheed, Killy na K-2GA.

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share.

About Author

Leave A Reply