Wednesday, August 21

WAZIRI MBARAWA: MIRADI 88 IMEJENGWA CHINI YA KIWANGO

0


Waziri wa Maji
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, amesema miradi 88 nchini imejengwa chini ya kiwango kati ya mwaka 2010 na 2015.

Mbarawa amesema hayo jana Mei 29, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (Chadema).

Katika swali lake Komu amesema kuna miradi imejengwa chini ya kiwango na kusababisha wananchi kutaabika kwa kukosa maji na kuhoji ni hatua gani ambazo serikali imechukua.

Akijibu swali hilo la nyongeza, Waziri Mbarawa alikiri kuwepo kwa miradi ya maji iliyojengwa chini ya viwango na kuongeza kuwa kati ya mwaka 2010 na 2015 miradi 88 nchini nzima ilijengwa chini ya kiwango.

Amesema nia ya serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanapata maji, hivyo hatua ya kwanza imekuwa ikikarabati vyanzo hivyo vya maji na kwamba imetengwa Sh milioni 135 kwa ajili ya ukarabati wa miradi hiyo. 

Share.

About Author

Leave A Reply