Wednesday, August 21

WAWILI WAFARIKI NA 17 KUJERUHIWA KATIKA SHAMBULIO LA KISU JAPAN

0


Watu wawili miongoni mwao akiwa mwanafunzi msichana, wameuawa kwa kudungwa kisu na mshambuliaji aliyewajeruhi watu wengine 17 nchini Japan jana. 

Mshambuliaji huyo aliwalenga wanafunzi wa shule waliokuwa wakisubiri basi. 

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka ya 50 na ambaye hajatambuliwa jina, aliwanyemelea wanafunzi hao kwenye kituo cha basi na kuwadunga visu, kisha naye akajidunga shingoni na kujiua. 

Polisi imesema msichana mwenye umri wa miaka 11 na mzazi mwenye umri wa miaka 39 na ambaye alitambuliwa kuwa afisa wa serikali walifariki kwenye shambulizi hilo ambalo limewashtua katika taifa ambalo visa vya uhalifu kama huo hutokea kwa nadra. 

Wengi wa waliojeruhiwa ni wanafunzi wenye umri wa miaka 12.

Share.

About Author

Leave A Reply