Wednesday, August 21

WABUNGE SABA WA CHADEMA KUVULIWA UONGOZI

0


Chadema

Kamati ya utendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini imemvua uanachama diwani wa Viti Maalum wa chama hicho, Digna Nassari kwa makosa ya kinidhamu. 

Kamati hiyo pia imependekeza Meya mmoja wa jiji anayetokana na chama hicho kuvuliwa uanachama kutokana na makosa ya kinidhamu na usaliti. 

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Mei 21, 2019 katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa amesema uamuzi huo umetolewa katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Mei 18, 2019. 

Amani mesema tayari uamuzi huo umepelekwa ngazi za juu za chama hicho sambamba na hatua za kinidhamu kwa wabunge saba. 

Amebainisha kuwa kikao hicho kiliongozwa na Kaimu mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Joseph Selasini ambaye ni mbunge wa Rombo. 

Chanzo: Mwananchi 

Share.

About Author

Leave A Reply