Saturday, August 24

SITA WAFARIKI KWENYE MAANDAMANO YA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI INDONESIA

0


Watu sita wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa mjini Jakarta nchini Indonesia, baada ya polisi wa kutuliza ghasia nchini humo kupambana na waandamanaji waliokuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi.

Baadhi ya Raia wa Indonesia wamekasirishwa na hatua ya Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo kumtangaza Rais Joko Widodo kuwa mshindi wa kiti cha Urais, kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Aprili mwaka huu.

Maeneo kadhaa ya mji wa Jakarta yamelazimika kufungwa baada ya ghasia kuendelea, huku waandamanaji wakiwa hawana dalili yoyote ya kusitisha maandamano yao.

Upande wa upinzani umekuwa ukidai kuwa, kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi wakati wa zoezi la kupiga kura nchini Indonesia, huku waangalizi wa Kimataifa wakitangaza kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.

Ushindi wa kishindo alioupata Widodo licha ya tuhuma hizo za upande wa upinzani, ndio umewatia hasira waandamanaji na kuamua kushiriki katika maandamano hayo yanayoambatana na ghasia. 

Share.

About Author

Leave A Reply