Tuesday, August 20

SERIKALI: AJIRA MPYA ZA SERIKALI HAZITAZINGATIA UZOEFU

0


Waziri ofisi ya waziri mkuu sera, kazi, ajira na walemavu

Serikali imesema imeanza kutekeleza program ya kuwaunganisha vijana wanaohitimu vyuo na taasisi mbalimbali ili kupata uzoefu kuepusha vijana wengi wanaohitimu kukosa ajira kwa kigezo cha kutokuwa na uzoefu licha ya kuwa na vigezo vingine.

Hayo yamesemwa na Waziri ofisi ya waziri mkuu sera, kazi, ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama akijibu swali kutoka kwa baadhi ya wabunge juu ya kuwepo kwa kigezo cha uzoefu katika kupata ajira wakati ndio wamemaliza masomo suala ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa vijana wengi wanaomaliza vyuo kukosa ajira

Naye Naibu waziri ofisi ya rais utumishi na utawala bora, Mary Mwanjelwa amesema ajira mpya za serikali zinazotolewa kuanzia sasa hazitozingatia suala la uzoefu kwa waajiriwa wapya hii ikiwa ni utekelezaji wa sera mpya ya utumishi 2004.

Mwanjelwa amesema mkakati huo unakwenda sambamba na kuhamasisha sekta binafsi kuajiri zaidi watanzania katika nyanja mbalimbali kulingana na sifa zinazohitajika ili kusaidia kuondokana na tatizo la ajira nchini. 

Share.

About Author

Leave A Reply