Thursday, August 22

RC HAPI ASITISHA LIKIZO ZA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI IRINGA

0


Mkuu wa mkoa wa Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa, Ally Happi.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amesitisha likizo za wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa halmashauri mkoani humo huku akiwataka kutosafiri nje ya Mkoa huo baada ya kufanya vibaya katika ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.

Hapi ametoa kauli hiyo jana Jumatatu Mei 27, 2019 wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri na kuwapa muda wa wiki tatu kuhakikisha wafanyabiashara wote wanapata vitambulisho hivyo.

Amebainisha lengo la Rais John Magufuli aliyegawa vitambulisho hivyo kwa wakuu wa Mikoa wote nchini ni kutaka wafanyabiashara wanatambuliwa na kuchangia maendeleo ya nchi kwa kulipa kodi.

Amewaonya watendaji wa vijiji na Serikali wanaodai kuwa vitambulisho vinasababisha mapato kupungua, akidai kuwa hiyo ni hoja dhaifu.

Hapi ameanisha makundi 53 ambayo yanastahili kupata vitambulisho hivyo, wakiwemo waandishi wa habari, wapiga debe, wauza mahindi, mchicha.

Amesema hakujiandaa kushindwa katika ugawaji wa vitambulisho na ndio sababu ya kusitisha likizo za viongozi hao ili wagawe vitambulisho hivyo ndani ya muda aliouweka ili Mkoa huo uweze kushika nafasi ya tatu katika ugawaji huo.

Kwa mujibu wa Hapi, Mkoa huo ni wa tano kutoka mwisho katika ugawaji huo wa vitambulisho. 

Share.

About Author

Leave A Reply