Thursday, August 22

RAPA RUSS ASHUSHWA JUKWAANI BAADA YA KUWATUKANA WAANDAAJI WA SHOW LAS VEGAS

0


Las Vegas

Rapper wa Marekani Russ amefukuzwa jukwaani pamoja na hotelini alipokuwa amefikia baada ya kuwatukana waandaaji wa show kwa ubovu kwenye matayarisho.

Russ ambaye na wimbo mpya aliomshirikisha Davido, alipanda stejini jijini Las Vegas wikendi iliyomalizika na kuanza kulalamikia production. Ghafla alishushwa jukwaani na kutolewa mizigo yake hotelini.

Kupitia ukurasa wake wa twitter aliandika kuwa watu wengine wapo kwa ajili ya kuona ukishindwa pasina kujali pesa za mashabiki waliokuja kutazama show, wanafanya vitu kwa ubaya ili baadaye aonekane msanii ndio kazingua na atupiwe lawana. Alimaliza Russ na kuwaahidi mashabiki wa Vegas kurejea na show yake mwenyewe na sio huu upuuzi. 

Share.

About Author

Leave A Reply