Sunday, August 18

NI WAZI SASA KUWA ADELE KAACHANA NA MUMEWE SIMON KONECKI

0


Mnamo jana mapema tu, Mitandao mbalimbali nchini Uingereza iliripoti kuwa mwimbaji na staa Adele ameachana na mumewe Simon Konecki. 

Wawili hao wameripotiwa kuachana kwa siri mwaka jana baada ya kudumu kwenye ndoa tangu mwaka 2016 lakini wamekuwa kwenye mahusiano kwa miaka 7. 

Wawili hao Pamoja walibarikiwa kuwa na mtoto mmoja wa kiume.

Imeelezwa kuwa Simon, mwenye umri wa miaka 45, anaweza kupata nusu ya utajiri wa mwimbaji huyo ambao unafikia (£150 million) sawa na Tsh. Bilioni 450.7

Tayari imewekwa wazi kuwa Adele aliuza jumba lao la kifahari lenye thamani ya (£3 million) lililopo nchini Uingereza mwezi February na akaingiza kiasi cha fedha kwenye akaunti ya Simon. 

Adele amebakiwa na majumba mengine matatu ya kifahari, moja ipo mjini Beverly Hills, nyingine ipo Kensington na ya mwisho ipo Southwest London. 

Share.

About Author

Leave A Reply