Tuesday, August 20

NAPE AIOMBA SERIKALI KUMRUHUSU CAG KUKAGUA MALIPO YA KOROSHO

0


Mbunge wa Mtama

Mbunge wa Mtama Nape Nnauye (CCM), amesema hali ya wakulima wa Korosho hivi sasa ni mbaya licha ya nia njema ya Rais kutaka wakulima wa zao hilo kulipwa, na badala yake zoezi hilo limetawaliwa na dhuluma pamoja rushwa, huku akibainisha kuwa zaidi ya wakulima 1181 bado mpaka sasa katika jimbo la Mtama hawajalipwa pesa zao.

Aidha Nape ameishauri Serikali kumruhusu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwenda kufanya ukaguzi katika zoezi hilo ili kuubaini ukweli, huku akitaka wale wote waliohusika katika mchakato wa uuzaji Korosho wawajibishwe kutokana na dhuluma wanaodaiwa kuifanya kwa wananchi wa mkoani Mtwara.

Wakati Nape akiyasema hayo Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini, amemshauri Spika wa Bunge Job Ndugai kuunda kamati ya wabunge wachache, kukagua maghala ya kuhifadhi Korosho, lengo likiwa ni kubaini Kororsho nzima na zilizooza.

Katika hoja yake mbunge huyo ambaye pia ni Kaimu Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, amesema zaidi ya asilimia 30 ya Korosho zimeoza.

Share.

About Author

Leave A Reply