Monday, August 26

MEEK MILL KUIBURUZA MAHAKAMANI COSMOPOLITAN HOTEL KWA UBAGUZI WALIOMFANYIA

0


Rapa Meek Mill

Meek Mill hajachukulia poa suala la ubaguzi wa rangu juzi mjini Las Vegas kwenye hoteli ya Cosmopolitan, mwanasheria wake ametupa taarifa kuwa atafungua shauri wiki hii dhidi ya hoteli hiyo.

Mwanasheria huyo Joe Tacopina ameiambia TMZ kwamba kwenye shauri hilo wataidai kiasi kikubwa cha pesa kwa uharibu, kudanganya na kumdhalilisha Meek Mill. Aliongeza kwa kuapa kwamba wanakwenda kuidondosha hoteli hiyo kwa walichokifanya.

Wiki iliyopita, Meek Mill alizuiliwa kuingia kwenye hoteli ya Cosmopolitan mjini Las Vegas, baada ya ku-post video akidai ubaguzi wa rangi umetawala.

Walinzi wa hoteli hiyo walimzuia Meek Mill kuingia kutokana na sababu walizozitaja kwamba hakufata utaratibu wa kuingia, hivyo watamkamata. 

Share.

About Author

Leave A Reply