Sunday, August 25

MAMLAKA ZA SRI LANKA ZAKATAZA UVAAJI WA ‘NIKAB’ KWASABABU ZA KIUSALAMA

0


Sri Lanka

Mamlaka Nchini Sri Lanka zimewazuia wanawake wa Kiislamu kivaa vitamba vinavyofunika uso(Nikab) kwaajili ya usalama

Uamuzi huu umechukuliwa ikiwa ni hatua ya kusaidia mamlaka kuwapata waalifu kwa urahisi. Wahalifu hao wanaotafutwa ni waliohusika kwenye mashambulio yaliyotokea siku ya Jumapili ya Pasaka na kuua zaidi ya watu 250

Uamuzi huu umezua hisia za tofauti miongoni mwa watu na zaidi ni kwa waumini wa dini ya kiislamu ambapo umoja wa waislamu Nchini humu umesema umetoa mwongozo kwa wanawake wa kiislamu kuheshimu maamuzi haya kwa muda kwani ni kwaajili ya usalama ila mamlaka zisijefikiria kufanya maamuzi haya kuwa ya moja kwa moja kwani hawatunga mkono

Share.

About Author

Leave A Reply