Monday, August 26

MALI ZA WANAOIKOSOA SERIKALI KUTAIFISHWA KUANZIA SASA

0


Mahakama kuu nchini Burundi na mwendesha mashtaka wa serikali wametoa amri ya kuzitaifisha mali za watu 41 wanaoikosoa serikali.

Watu ambao wameathirika na tamko hilo ni wanasiasa wa zamani, wanaharakati wa haki za kibinadamu na waandishi wa habari, pamoja na afisa wa jeshi ambao wamefungwa jela nchini humo.

Tarehe 15 May, wametakiwa kuwasilisha mali zao na kuteketezwa na serikali.

Hatua hiyo imekosolewa na kudaiwa kuwa njama nyingine ambayo serikali ya Pierre Nkurunziza ya kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2020.

KWANINI WATAIFISHWE SASA? 

Amri ya mahakama imekuja baada ya miaka minne tangu walivyokwenda kinyume na serikali na hata mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mwakani 2020.

Awali rais Nkurunziza alidai kutogombea tena wadhfa huo lakini mpaka sasa si yeye wala chama chake wamemtaja mgombea ambaye atachukua nafasi ya Nkurunziza.

Siku za hivi karibuni, chama kikuu cha upinzani cha nchini humo CNL kimekutana na changamoto kutoka katika mamlaka na vijana.

Jambo ambalo liliwakasirisha wapinzani ambao walikutana katika mkutano tarehe 3 mpaka 5 Mei.

Madhumuni ya kikao hicho ambacho kilifanyika Uganda, kilikuwa kinalenga kupanga mikakati ya namna ambavyo vyama vya upinzani vinaweza kuungana na kupambana na chama kinachotawala katika uchaguzi utakaofanyika 2020.

Wakati machafuko yaliyotokea Burundi mwaka 2015 bado hayajasahaulika, jambo ambalo lilimfanya Nkurunziza kutoa maamuzi ya kutogombea tena ili kutovunja makubaliano ambayo alisaini mwaka 2000.

Nchi hiyo ikiwa inakabiliwa na migogoro ya kiuchumi kwa muda mrefu. Mei 15, baadhi ya wabunge waliikosoa serikali kwa kutumia vibaya fedha ambazo ziliwekwa katika bajeti ya taifa.

Kutaifishwa kwa mali za wakosoaji wa serikali kunaweza kuwa na lengo la kusawazisha mapungufu yaliyojitokeza katika bajeti ya kitaifa, jambo ambalo limepelekea nchi kuwekewa vikwazo kimataifa na kupunguza misaada ya kigeni

WAKOSOAJI WAMESEMAJE? 

Baadhi ya watu ambao wameathirika na hatua hiyo wameonyesha hasira yao kwenye mitandao ya kijamii.

“Tayari tuko uhamishoni, nini zaidi wanakitaka kwa kuchukua mali zetu kidogo tulizoziacha Burundi?”

Jarida la habari linalotoka kila wiki ‘Jeune Afrique’ lilimnukuu kiongozi wa upinzani nchini Burundi ambaye yuko uhamishoni Alexis Sinduhije.

“Kama lengo ni kutuvunja moyo basi wameshindwa! Jambo hilo halitabadilisha nia yetu.

Kama ni namna ambayo inathibitisha simulizi yao ya ujinga basi ni mafanikio!

Kama hiyo ndio namna ya kuonyesha kiwango cha chuki walichokuwa nacho, basi tayari tumeshajua” mwanaharakati wa haki za binadamu aliyekuwa uhamishoni.

“Pierre Nkurunziza na wafuasi wake wanaendelea na mchakato wa kutaifisha mali zao.

Ni maamuzi ambayo yako wazi kwa ajili ya kutoa ufafanuzi.

Ni kitu chochote lakini ndio maamuzi ya mahakama,” alisema Vital Nshimirimana, kiongozi mwingine wa upinzani ambaye yuko uhamishoni .

KITU GANI KINATARAJIWA KUTOKEA? 

Hatua ya kuchukua mali za wakosoaji wa serikali inaonekana kutoendana na watuhumiwa ambao wameshutumiwa kuvunja sheria katika serikali .

Hii ni dalili ya kuanzisha harakati zake za kudhoofisha upinzani kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Amri ya mahakama inaonekana kuwa inataka kuwakatisha tamaa viongozi wa upinzani na wakosoaji wa serikali kutorudi Burundi mwakani kwa ajili ya uchaguzi. 

Share.

About Author

Leave A Reply