Wednesday, August 21

MAHAKAMA KUU YAAMURU KURA KUHESABIWA UPYA MALAWI

0


Malawi General Election

Mahakama Kuu imeiamuru Bodi ya Uchaguzi kutotangaza matokeo ya Urais hadi kura kutoka kwenye theluthi ya Majimbo zirudiwe kuhesabiwa

Hii ni baada ya chama kikuu cha upinzani, Malawi Congress Party(MCP) kwenda kushitaki wakidai kuwepo hali ya sintofahamu katika matokeo ya majimbo 10 kati ya 28 yaliyopo

Vyama vingine vya upinzani pia vililalamikia kubadilishwa kwa namba kwenye karatasi za matokeo kwa kutumia wino wa kufutia na mwandiko mmoja kukutwa kwenye karatasi za vituo vilivyo na umbali mkubwa kati yao.

Mgombea mwingine ambaye ni Makamu wa Rais, Saulos Chilima amesema uchaguzi huo umegubikwa na ukosefu wa haki na udanganyifu na kuomba ufutwe

Hadi Alhamisi Mei 23, Matokeo yaliyotangazwa yalionesha Rais Peter Mutharika akiongoza kwa 40.9% huku mpinzani wake wa karibu, Chakwera wa MCP akiwa na 35.44% na Chilima akiwa na 18% ya kura zilizohesabiwa.

Waangalizi kutoka Umoja wa Ulaya walielezea uchaguzi huo uliofanyika Mei 21 kuwa “ulioendeshwa vema, wa uwazi na ushindani mkubwa”

Share.

About Author

Leave A Reply