Wednesday, August 21

‘MAESTRO’ XAVI AANZA KAZI YA UKOCHA RASMI

0


Kiungo wa zamani wa klabu ya FC Barcelona inayoshiriki LALIGA, na timu ya Taifa ya Hispania, mhispania Xavi Hernandez ameajiriwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Al Sadd ya nchini Qatar kwa mkataba wa miaka miwili. 

Xavi, 39 alifanikiwa kucheza michezo 767 kwa FC Barcelona na michezo 113 kwa timu yake ya taifa la Hispania kabla ya kuhamia klabu ya Qatar mwaka 2015. 

Mapema mwezi huu Xavi alitangaza kustaafu kucheza kandanda moja kwa moja na kwa sasa angejishughulisha na shughuli nyingine. 

Habari hii inakwenda tofauti na matarajio ya mashabiki wengi wa FC Barcelona ambao wangetamani kuona Xavi anarudi klabuni hapo sasa hivi kuokoa jahazi la timu yao linalopigwa na mawimbi mengi ya uchungu wa kupoteza kizembe michezo kwenye ligi ya mabingwa Ulaya. 

Katika mahojiano na moja ya vituo vya televisheni vya Qatar, Xavi alipoulizwa kuhusu kurudi Barcelona alisema kuwa hawezi kurudi kwa sasa, labda baada ya miaka 2 mbele. 

Share.

About Author

Leave A Reply