Wednesday, August 21

KIPINDUPINDU TISHIO JIPYA DAR, CHAUA MTU MMOJA HUKU 32 WAKILAZWA

0


Mtu mmoja amefariki dunia kwa kipindupindu jijini Dar es Salaam huku wengine 32 wakilazwa katika kambi maalum. 

Hayo yamesemwa jana Jumatano Mei 29, 2019 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake jijini Dar es Salaam kuangalia hali ya ugonjwa wa kipindupindu na homa ya Dengue.

“Tumepokea wagonjwa 32 katika mkoa wa Dar es Salaam, kambi ya Amana wapo 13, Temeke 18 na Mwananyamala mgonjwa mmoja, hii ni kutokana na hali halisi ya kutozingatia usafi,” amesema.

Kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo, Waziri Ummy ametoa amezitaka halmashauri zote za mkoa wa Dar es Salaam kutoa sheria kali kwa wanaotiririsha maji machafu wakati wa mvua.

“Mstahiki Meya kasema adhabu ni Sh 30,000 nimewataka waongeze adhabu iwe Sh 200,000 tunataka mtu aone ni bora kuita gari la maji taka Sh 150,000

kuliko kulipa hiyo faini nimeshatoa maagizo yeyote atakayetiririsha maji machafu atachukuliwa hatua kali,” amesema Ummy.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Yudas Ndungile amesema sehemu kubwa ya wagonjwa wa kipindupindu waliopatikana wanatoka eneo la Mchikichini na mabondeni ambako magari ya kusomba taka hayapo, “Mipango inafanywa kuangalia namna ya kuyafikia hayo maeneo.”

Share.

About Author

Leave A Reply