Wednesday, August 21

KAMPUNI YA GOOGLE YATANGAZA KUACHA KUFANYA KAZI NA KAMPUNI YA HUAWEI

0


Google to not work with Huawei anymore

Leo mapema uko USA kampuni kubwa ya technology duniani google au unaweza kuiita alphabet, imetangaza kuacha kufanya kazi na kampuni ya kichina ya Huawei.

Google wamesema simu zote za Huawei za zamani zitaendelea kupata technical support yaani android operating system, kwa muda fulani lakini hazitaweza kufanya Updates kwa versions mpya za android, zitabaki hivyo hivyo.

Simu zote mpya za Huawei (smartphones) hazitaweza kutumia tena android operating system,na huduma zingine kutoka kampuni ya google mfano YouTube,na apps nyinginezo zilizopo kwenye android phones.

Hii inamaana Huawei wataathirika Sana sokoni maana dunia imekuwa addicted na android operating system au iOS,na bado social media giants Kama facebook hawajaanza kufuata order.

Japo Huawei wamesema washaandaa operating system zao, na components zingine ambazo walikuwa wanategemea kutoka USA,je dunia inaweza kuanza kutumia social media na operating system za kichina na kuachana na USA au ni kifo cha Huawei? 

Kumbukeni china na wao walisha wapiga ban google na social media giants companies za USA ku operate ndani ya china,je hii vita nani atashinda?

Kwa wale wanaotumia na mko addicted na Huawei smartphones, nadhani ni wakati mwafaka mjiandae either kuanza kujifunza kichina maana mtaanza kutumia social media za kichina na operating system za kichina au mnunue simu zingine Ha hahaha hahaaaaaa. 

Share.

About Author

Leave A Reply