Thursday, August 22

KAMPUNI YA BOEING YAKIRI KUWEPO HITILAFU KWENYE ‘SOFTWARE’ YA 737 MAX

0


Hitilafu software ya Boeing 737 Max

Kampuni ya uundaji ndege ya Boeing imekiri kuwa imelazimika kurekebisha makosa kwenye “software” ya 737 MAX inayotumika kufundishia marubani baada ya ajali mbili zilizoua jumla ya watu 346

Katika taarifa yao wamesema wameongeza taarifa zaidi kwa waongoza ndege ili kuhakikisha inafaa katika hali tofauti za safari

Licha ya kukiri huko Boeing haikusema ni lini waligundua tatizo hilo lililosababisha ajali ya ndege ya Ethiopia mwezi Machi, 2019 na ile ya Lion Air Oktoba, 2018 na wala kusema endapo waliwajulisha waratibu.

Ndege hizo zimesitishwa matumizi duniani kote zikisubiri ruhusa kutoka Marekani na waratibu wa kimataifa kabla ya kuanza kutumika tena. 

Share.

About Author

Leave A Reply