Sunday, August 18

INSTAGRAM INA MPANGO WA KUONDOA KABISA UWEZO WA KUONA LIKES KWENYE POSTS

0


Huenda kuna siku ukaamka na usione LIKES kwenye picha za watu au mastaa uliowafata kule instagram kwani imeripotiwa kuwa mtandao huo una mpango wa kuanza kuficha kipengele hicho muhimu. 

Kwa mujibu wa mwanadada mmoja ambaye anafahamika kama Jane ametudokeza juu ya uwezekano huo huku akituonesha jinsi itakavyokuwa. Mtumiaji hataweza kuona idadi ya LIKES kwa picha atakayokutana nayo kwenye uso wake (Feed) bali yule aliye-share tu ndio anaweza kuona idadi hiyo.

Kupata uhakika, mtandao wa The Verge uliamua kuwatafuta instagram ili kupata taarifa rasmi: Walisema kuwa hawapo kwenye majaribio yoyote lakini wanatafuta namna ya kupunguza presha kwenye instagram, ni kitu wanacho kifikiria.”

Ajenda hii iliwahi kuletwa mezani na Kanye West kupitia ukurasa wake wa twitter September 22, 2018. 

Share.

About Author

Leave A Reply