Thursday, August 22

BOW WOW AWATOLEA UVIVU ‘MADEMU WALA BATA WA INSTA’

0


Bow wow

Najua umeshawahi kuwatazama na kujiuliza mengi kuhusu mademu wa mitandaoni jinsi wanavyokula bata pamoja na hali za uchumi kutokuwa njema kwa wengi wetu. Swali kubwa huwa ni kwa namna gani warembo hao wa mitandaoni wanaingiza mkwanja? Bow Wow ameungana na sisi kujiuliza swali hilo. 

Kwenye insta story yake, Bow Wow amezungumza kwamba hawa warembo wa instagram hawana mkwanja wowote na maisha wanayoishi kwenye mitandao ni FAKE. 

“Umewahi kugundua namna warembo wa IG wanavyokula bata na kwenda mapumzikoni (Vacation) kuliko kawaida? Yani huna gari, huna nyumba lakini upo Dubai wiki hii na Uturuki wiki ijayo. Nani analipia upuuzi huu? Na hawajawahi kutuonesha mabwana zao, wanajifanya wapo na wanawake tu. Acheni hizo. Tiketi ya ndege ni ($2K) na zaidi ukijumlisha na hoteli. Tunajua hamlipii hivi vitu.” alisema Rapper Bow Wow. 

Povu hili liwaendee wahusika…

Share.

About Author

Leave A Reply