Saturday, August 24

BAKWATA: MAADHIMISHO YA EID EL FITR KITAIFA KUFANYIKA TANGA

0


Taarifa rasmi ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) iliyotolewa leo, Alhamisi, imesema kuwa sikukuu hiyo itafanyika kulingana na mwandamo wa mwenzi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza Baraza la Eid litakalofanyika mkoani Tanga ambako ndiko sherehe hizo zitaadhimishwa kitaifa mwaka huu.

“Swala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti Mkuu wa wa Ijumaa uliopo Barabara ya 10 Ngamiani Tanga Mjini kuanzia majira ya saa 1:30 asubuhi,” imeongeza taarifa hiyo.

Mufti na Sheikh Mkuu, Abubakar Zubeir bin Ally amewataka Waislamu na wananchi wote nchini kusherehekea sikukuu hiyo kwa usalama na amani.

Share.

About Author

Leave A Reply