Tuesday, August 20

Video: Sumu ya panya inavyotumiwa kama dawa ya kulevya Tanzania

0


Matumizi ya dawa za kulevya nchini Tanzania yamechukua sura mpya, kufuatia baadhi ya watumiaji wa dawa hizo, kuanza kutumia sumu ya kuua panya, kama sehemu ya kilevi.

Watumiaji hao wameeleza kuwa dawa ya hiyo ya panya ambayo huchanganywa na dawa nyingine, inakuwa ni tamu kuliko dawa za kulevya zinazofahamika za heroine na cocaine.

Watumiaji wa dawa hizo huenda wametafuta njia hiyo rahisi ya kukata kiu zao ama kwa vile dawa za kulevya ni ghali au zimeadimika nchini Tanzania kufuatia hatua mbalimbali ambazo zimechukuliwa na serikali kukabiliana nazo.

Waraibu (watumiaji) wa dawa za kulevya, ambao wanafahamika kwa jina la mateja nchini Tanzania sasa wanachanganya sumu hiyo ya panya na dawa nyengine kulevya kama vile bangi na kisha kuvuta pamoja.

Wataalamu wa afya wameeleza kuwa, matumizi ya sumu hiyo kama kilevi ni hatari zaidi ya dawa za kulevya za asili kama Coccaine na Heroine, kwani mtumiaji akizidisha kiwango, anaweza kufa hapo hapo kwa sababu ni sumu.

Share.

About Author

Leave A Reply