Monday, August 19

Utafiti: Tanzania yaongoza Afrika kwa wananchi kuwa na msongo wa mawazo

0


Kwa kuetegemea na eneo unaloishi, msongo wa mawazo unaweza kusababishwa na mambo mbalimali kama vile mapigano, njaa na matatizo mbalimbali au mtatizo ya mazingira yako unayofanyia kazi.

Hali hiyo huwakumbua wananchi wote, kutoka katika nchi zinazoendelea au zile zilizoendelea.

Taasisi ya Gallup imefanya utafiti wa kuangalia kiwango cha msongo wa mawazo katika nchi 143 duniani ikiwa ni sehemu ya 2019 Global Emotions Report ambapo zaidi ya robo tatu ya waliohojiwa walisema kuwa walikumbana na mazingira ya kuwasababishia msongo wa mawazo, siku moja kabla ya utafiti huo.

Katika ripoti hiyi iliyochapishwa na jarida la Forbes, Ugiriki ndio inaongoza kwa kuwa na wananchi wenye msongo wa mawazo ikiwa na asilimia 59, ambapo msongo huo unachangiwa kwa kiasi kikubwa na kuporomoka kwa uchumi wa nchi hiyo.

Nafasi ya pili inashikiliwa na Ufilipino ikiwa na asilimia 58, huku Tanzania yenye asilimia 57 ikiwa nchi ya kwanza kutoka Afrika katika orodha hiyo.

Kutoka Afrika (Mashiriki) katika orodha ya nchi 10 zenye msongo zaidi kuna nchi tatu ambazo ni Tanzania, Uganda na Rwanda.

Utafiti huo ukitolea mfano wa Marekani ambayo imo miongoni mwa nchi 10 ambazo raia wake wana msongo wa mawazo imeeleza kuwa, viwango vya tatizo hilo vimekuwa vikiongezeka kwa nchi mbalimbali duniani.

Mwaka 2006, raia 46% wa Marekani ndio walikuwa na msongo wa mawazo, idadi iliyoongezeka na kufikia asilimia 53 mwaka 2014, na sasa ni asilimia 55.

Utafiti huo umeeleza kuwa watu wenye umri wa kati ya miaka 15 na 49 ndio waathirika wakubwa.

Share.

About Author

Leave A Reply