Sunday, August 18

Tigo Pesa inavyotoa ajira kwa maelfu ya Watanzania

0


Nchini Tanzania, watu wengi sasa wanaweza kutuma na kupokea fedha kupitia simu za mkononi wakiwa mahali popote pale, na yote haya yamewezeshwa kwa kuenea kwa teknolojia ya mitandao ya simu kama Tigo.

Kupitia huduma ya Tigo Pesa, wananchi wanaweza kutuma na kupokea fedha kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki. Lakini pia kwa kutumia Tigo Pesa wananchi wanaweza kufanya malipo mitandao, kwa kulipia huduma na bidhaa mbalimbali.

Mbali ya unafuu wote huo ulioletwa na Tigo Pesa ambapo unaweza kuyakamilisha hayo yote na mengine ukiwa umepumzika ndani kwako, bado Tigo Pesa imeweza kutoa ajira kwa watu na makampuni mbalimbali, ikiwa ni njia ya kuendelea kuisaidia jamii.

Miongoni mwa njia nyingi ambazo ajira zimepatikana kupitia Tigo Pesa ni uwakala ambapo nchini nzima kuna zaidi ya mawakala 100,000. Kupitia mawakala hawa, unaweza kutuma na kutoa fedha wakati wowote, lakini pia kulipia huduma na bidhaa.

Kutokana na miamala ambayo mawakala hawa huifanya, nao huweza kujiingizia kipato, ambapo watu wengi wametumia ajira hiyo kuboresha maisha yao.

Mbali na uwakala, Tigo Pesa imetoa ajira kwa watu na makampuni mbalimbali ambayo hubuni na kutengeneza matangazo na bidhaa tofauti kwa ajili ya kutangaza huduma za Tigo ikiwemo wasanii.

Makampuni mbalimbali na watu hutumiwa katika kutangaza huduma za Tigo Pesa na kupitia njia hiyo, wafanyakazi katika makampuni hayo, huweza kujiingizia kipato, lakini pia serikali hupata mapato kupitia shughuli hizo.

Aidha, Tigo Pesa ametoa ajira kwa wataalamu wa kompyuta ambao husimamia mifumo ya mawasiliano kuhakiki huduma bora zinapatikana wakati wote.

Wataalamu hawa hawa huhakikisha kuwa wateja wanaweza kutuma na kupokea fedha pamoja na kulipia bidhaa na huduma nyinginezo muda wote, kwa urahisi na usalama wa hali ya juu wa pesa zao.

Haya yote na mengine yanadhihirisha kuwa tu Tigo Pesa ni zaidi ya Pesa, kwani manufaa yake kwenye jamii hayaishii tu kutuma na kupokea fedha, bali yanaboresha maisha ya Mtanzania mmoja mmoja, na kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko chanya kwenye jamii.

Share.

About Author

Leave A Reply