Sunday, August 25

Tanzania yalizuia Shirika la Fedha Duniani (IMF) kuchapisha ripoti ya uchumi

0


Tanzania imetumia kura yake ya veto kuzua kuchapishwa kwa ripoti inayoihusu ambayo huandaliwa na Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Ripoti hiyo ya IMF (Article IV report) huangazia kwa kina hali ya uchumi ya nchi husika pamoja na sera zinazohusu ubadilishaji wa fedha za kigeni. Ripoti hiyo inahusisha uchambuzi wa kina wa uchumi wa nchi husika na mikakati ya kisera.

Aprili 17, 2019, IMF ilitoa taarifa ikieleza kuwa serikali ya Tanzania imezuia kuchapishwa kwa ripoti hiyo ambayo tayari maandalizi yake yalikwisha kamilika.

Kwa mujibu wa sheria za IMF. serikali ya nchi husika ni lazima iridhie kwanza ndipo ripoti hiyo na nyaraka nyingine zinayohusiana nazo zichapishwe.

Katika taarifa hiyo IMF imeeleza kuwa Bodi ya Wakurugenzi ilikamilisha mapitio ya ripoti hiyo iliyowasilishwa kwao Machi 18 mwaka huu.

Katika kuandaa ripoti hiyo, maafisa kutoka IMF hutembelea nchi mwanachama, mara moja kwa mwaka, kukusanya taarifa, kufanya majadiliano na maafisa wa serikali na benki kuu katika nchi hizo.

Wanaporejea, maafisa hao huwasilisha ripoti kwa Bodi ya Wakurugenzi, ambapo maoni ya bodi huandikiwa mukhtasari na kisha kutumwa kwa nchu husika.

Mara ya mwisho IMF kuaandaa ripoti kama hiyo (Article IV report) ni mwaka 2016 ambapo serikali iliruhusu ripoti hiyo kuchapishwa.

Uamuzi wa Tanzania kuzuia ripoti hiyo inakuja wakati serikali imekuwa ikikosolewa kutokana na sera zake ambalimbali ambazo zinadaiwa kuwa si rafiki kwa ukuaji wa uchumi na sekta binafsi.

Lakini pia hatua hiyo imekuja siku chache kufuatia IMF kupunguza makadirio ya kiwango cha ukuaji wa uchumi wa Tanzania kutoka asilimia 6.6 iliyokuwa imesema awali hadi asilimia 4, kwa mwaka 2019.

Share.

About Author

Leave A Reply