Sunday, August 25

Serikali yafuta sherehe za maazimisho ya Muungano (Aprili 26)

0


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema leo tarehe 26 Aprili, 2019 ni siku ya mapumziko na hakutakuwa na shamrashamra za sherehe.

Akizungumza ofisini kwake jijini Dodoma Alhamisi, Aprili 25, 2019, Waziri Mkuu alisema kesho (leo) ni siku ya mapumziko kitaifa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lakini hakutakuwa na sherehe.

Amesema jumla ya sh. milioni 988.9 ambazo zilikuwa zimepangwa kwa ajili ya sherehe hizo, zimeokolewa na zitapangiwa shughuli nyingine.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Share.

About Author

Leave A Reply