Sunday, August 25

Samatta aongoza kwa magoli barani Ulaya

0


Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika Klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji anashikilia usukani wa magoli miongoni mwa wachezaji kutoka Afrika wanaosakata soka barani Ulaya.

Mbwana Samatta, ukipenda muite Samagoal ambaye amejiziloea umaarufu na ushawishi kufuatia kauli yake ya Haina Kufeli tayari ametundika kambani magoli 31 katika msimu huu kwenye mashindano yote.

Akiwa na magoli 31, Samatta amewaacha mbali wachezaji wenzake kutoka Afrika, ambapo mchezaji anayefuatia ni Mo Salah wa Liverpool na Pierre Aubameyang wa Arsenal ambapo kila mmoja ana magoli 23.

Mbali na kutundika kambani magoli 31, Mbwana Samatta amekuwa na usaidizi (assists) katika magoli sita.

Hakim Ziyech kutoka Morocco anayekipiga katika Klabu ya Ajax ndiye mwenye ‘assists’ nyingi zaidi, ambapo amekuwa na mchango katika magoli 20 hadi sasa, huku akifunga magoli 19.

Hapa chini ni orodha ya wachezaji 10 kutoka Afrika wanaoongoza kwa magoli barani Ulaya katika mashindano yote.

Mchezaji Nchi Usaidizi (assists) Magoli
Mbwana Samatta Tanzania 6 31
Mo Salah Misri 11 23
Pierre Aubameyang Gabon 7 23
Sadio Mane Senegal 3 22
Lars Veldwijk Afrika Kusini 5 21
Nicolas Pépé Ivory Coast 14 20
Hakim Ziyech Morocco 20 19
Abdenasser El
Khayati
Morocco 11 17
Ishak Belfodil Algeria 5 14
Wahbi Khazri Tunisia 8 14

Kufuatia uwezo huu wa wachezaji wa Afrika kufanya vizuri barani Ulaya, wengi wanaamini kuwa fainali zijazo za Mataifa ya Afrika ambazo Tanzania pia itashiriki nchini Misri zitakuwa na ushindani mkali, kwani zitawakutanisha wababe kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika.

Share.

About Author

Leave A Reply