Tuesday, August 20

RC Iringa apiga marufuku wagonjwa kutundikiwa dripu bila kupimwa

0


Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amepiga marufuku tabia ya hospitali mkoani humokuwachoma sindano wagonjwa na kuwatundikia dripu kabla ya kuwapima.

Hapi amesema tabia hiyo amayo ameeleza kuwa ni uozo haiweze kukubalika katika mkoa huo, na ameagiza tabia hiyo kukomeshwa mara moja.

Uozo huu nataka usafishwe. Sitaki kusikia mambo haya kwenye hospitali zote za Mkoa wa Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ziarani mkoani humo amesema kwamba hawatakuwa na huruma na mtu yeyote atakayebainika kufanya hivyo, awe ni daktari, muuguzi au mhudumu yeyote wa afya.

Baadhi ya watu wameonesha kutofurahishwa na kuali hiyo, wakisema kwamba, suala hilo ni la kitaalamu na kiongozi huyo hana taaluma husika, hivyo ni vyema akaliacha kwa wanaoelewa.

Hamis Kigwangala plz call this man tell him @AllyHapi you don’t need investigation/laboratory findings kumuwekea mtu drip…….. mpe idea, maana aliloliongea hapa ni aibu. Ameandika, @JrKinubi

@geodonny ameandika, AllyHapi Bro ulishawahi kuwa Daktari?, Unajua protocol za kitabibu zilivyo?, Hao madaktari wa hapo Iringa wakikuambia uwaonyeshe jinsi ya kutibu utaweza? Unapoamua kuongelea taaluma ambayo huijui bas chunga maneno yako?

Mkuu AllyHapi nimekuskiliza kwa makini katika mahojiano yako na vyombo vya habari baada ya kutembelea hospitali Iringa kwamba Mgonjwa hatakiwi kuwekewa drip kama hajapimwa. Mimi ni nurse by professional, Kabla sijakuuliza mkuu je una uelewa wowote wa maswala ya Afya? Nisikuonee. Ameandika @TreshaMpare

Share.

About Author

Leave A Reply