Monday, August 19

Nyoka wamkimbiza Rais ofisini

0


Noka wamepatikana katika ofisi ya Rais wa Liberia, George Weah, na hivyo kumlazimu kufanya kazi kutoka katika makazi yake binafsi.

Mkuu wa Mawasiliano, Smith Toby amesema kuwa siku ya Jumatano, nyoka wawili weusi walipatikana katika Jengo la Wizara ya Mambo ya Nje, ambapo ndipo ilipo ofisi ya kazi ya Rais.

Kufuatia hatua hiyo, watumishi wote wanaotumia jengo hilo wametakiwa kutofika kazini hadi Aprili 22 wakati dawa ya kuua wadudu ikifukizwa katika jengo hilo.

Ofisi ya Rais imekuwa ndani ya jengo la Wizara ya Mambo ya Nje tangu mwaka 2006 baada ya moto kuteketeza makazi ya Rais yaliyopo jirani na jengo hilo.

Smith Toby amesema kuwa nyoka hao baada ya kuonekana hawakuuawa, badala yake waliingia katika shimo dogo lililopo kwenye jengo hilo.

Polisi na Kitengo cha Ulinzi wa Rais kilionekana kikilinda makazi ya Rais yaliyopo katika Mji Mkuu wa nchini hiyo, Monrovia.

Jengo la Wizara ya Mambo ya Nje limekuwapo kwa miaka mingi sana, hivyo kutokana na mfumo wa kukausha maji, uwepo vitu kama nyoka ni mkubwa, alisema Toby.


Aidha, Toby alisema kuwa Rais atarudi katika ofisi yake Jumatatu hata kama nyoka hao watakuwa hawajapatikana na kuuawa.

Share.

About Author

Leave A Reply