Tuesday, August 20

Natamani niwe Waziri wa Michezo, timu nitapanga mimi- Rais Magufuli

0


Rais Dkt John Pombe Magufuli ameoneshwa kuchukizwa kwake na kitendo cha timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, kupoteza michezo yake yote mitatu.

Serengeti Boys ilifungwa michezo yote mitatu katika Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya miaka 17 (AFCONU17). Katika mchezo wa kwanza ilifungwa na Nigeria (4-5), ikafungwa na Uganda (3-0), kabla ya kufungwa mchezo wa mwisho na Angola (2-4).

Rais Magufuli akizungumza na wakazi wa Kyela mkoani Mbeya amesema inashangaza sana kuona timu ipo katika uwanja wake, imeandaa mashindano yenyewe lakini inafungwa hovyo.

Amesema kuwa kwenye hilo waziri mwenye dhamana, Dkt Harrison Mwakyembe amemwangusha na kwamba hio aibu ataibeba yeye, na hajui ataifuta lini.

Aidha, Rais aligusia pia fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka huu ambayo pia Tanzania itashiriki nchini Misri mwezi Juni. Amesema, si ajabu hata katika mashindano hayo, timu ya Tanzania ikafungwa katika mchezo wa kwanza.

Natamani siku moja niwe waziri wa michezo halafu waone mimi watakavyokuwa, timu nitaipanga mwenyewe, lakini ndio hivyo, alisema Rais.

Katika fainali za AFCONU17, Tanzania ilitolewa katika hatua za makundi, na hivyo kushindwa kufuzu kushiriki Kombe la Dunia la U-17, fainali zitakazofanyika mwaka huu nchini Brazil.

Share.

About Author

Leave A Reply