Sunday, August 18

Msimamo wa serikali kuhusu kuongeza mishahara ya wafanyakazi

0


Serikali imesema kuwa inafahamu kuhusu suala la kupandisha mishahara ya watumishi, na kwamba itafanya hivyo wakati ukifika.

Kauli hiyo ilitolewa na mawaziri watatu tofauti bungeni ambao ni Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama na Naibu Waziri wa Elimu, William Ole Nasha.

Viongozi hao walikuwa wakijibu hoja ya Mbunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA Ruth Mollel aliyeitaka Serikali kuongeza mishahara ya watumishi.

Waziri George Mkuchika alisema kuwa serikali inajenga reli ya kisasa (SGR), kukarabati na kujenga viwanja vya ndege, na miradi mingine mikubwa na kwamba wakati ukifika watumishi wataongezewa mishahara yao, kwani serikali inalifahamu hilo.

Unataka standard gauge, kukarabati kwanza uwanja wa ndege. Muda utakapofika tutatoa nyongeza mishahara. Walio na dhiki na uwanja wa ndege wangesema tupe ndege kwanza, alisema Waziri Mkuchika

Tuna muda wa kukaa kujadiliana, Serikali itatekeleza kila jambo kwa wakati sahihi, alisema Waziri Mhagama akisisitiza kusudio lake la kukutana na kufanya mazungumzo na vyama vya upinzani kuhusu suala hilo.

Share.

About Author

Leave A Reply