Monday, August 19

Mbunge aihoji serikali kuhusu ongezeko la watu kukosa nguvu za kiume

0


Mbunge wa Ulanga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ameihoji serikali leo bungeni kuhusu ongezeko la dawa za kuongeza nguvu za kiume nchini, huku akitaka kujua kama kuna utafiti wowote umefanya kuweza kufahamu sababu ya ongezeko hilo.

Goodluck Mlinga amesema kwa siku za karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya dawa hizo, kama vile Supermoringe, Supergafina, Jasosi Mix, Amsha Mzuka, Sado Power na Congo Dust, ambayo imeonesha mafanikio makubwa.

Amesema kuwa zamani ilizoeleka watu kutumia mkuyati kama dawa ya kuongeza nguvu za kiume, lakini sasa kumekuwa na lundo la dawa hizo, hivyo akataka kujua sababu za watu kukosa nguvu za kiume.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Hussein Mwinyi amesema kuwa kuna dawa zilizothibitishwa na mamlaka husika zinazoweza kutumiwa kuongeza nguvu za kiume na hazijaonesha kuwa na madhara kwa watuamiaji.

Waziri Mwinyi amesema kuwa dawa hizo zinauzwa kihalali na kushauri kwamba, wale wote wanaotaka kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume watumie zilizopitishwa na mamlaka za udhibiti, na sio ambazo hazijathibitishwa, ili kuepuka madhara ya kiafya.

Share.

About Author

Leave A Reply