Friday, August 23

Mapato ya Acacia yaporomoka kwa TZS bilioni 46

0


Mapato ya kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia (Acacia Mini Plc) yameendelea kupungua, wakati ikiendelea kukabiliana na changamoto za uzalishaji katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara nchini Tanzania.

Mapato ya kampuni hiyo kwa miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2019 (iliyoishia Machi 31) kabla ya kodi na makato mengine ni TZS bilioni 55.3 ($24 milioni), ambapo imeshuka kutoka TZS bilioni 101.4 ($44 milioni) katika kipindi cha mwaka 2018.

Uzalishaji wa dhahabu imeshuka kwa asilimia 13 hadi tani 2.973 (104,899 ounces) katika robo ya kwanza ya mwaka 2019. Hii ilitokana na mmomonyoko wa ardhi katika eneo la mgodi, North Mara, na kuzuia shughuli za uchimbaji.

Mbali na changamoto za uchimbaji, kampuni hiyo pia inakabilia na changamoto za kodi nchini Tanzania ambapo ndipo migodi yake yote ilipo.

Aidha imepunguza uzalishaji tangu serikali ya Tanzania ilipozuia usafirishaji wa makinikia mwaka 2017.

Katika taarifa nyingine Acacia imesema kuwa Mike Kenyon na André Falzon wataondoka katika bodi ya kampuni hiyo na kwamba wamewateua
Alan Ashworth, Deborah Gudgeon na Adrian Reynolds ambao si sehemu ya menejimenti (independent non-executive directors).

Share.

About Author

Leave A Reply