Friday, August 23

Kimbunga Kenneth kutua Mtwara Ijumaa alfajiri

0


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo mchana imetoa taarifa mpya juu ya mwenendo wa Kimbunga Kenneth na kusema kuwa kinatarajiwa kutua Ijumaa alfajiri au asubuhi katika Pwani ya Mtwara.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt Agness Kijazi alisema hadi kufikia saa tisa leo alasiri kimbunga kingekuwa umbali wa kilomita 177 kutoka pwani ya Mtwara kikiwa na kasi ya kilometa 140 kwa saa.

Licha ya kuwa kimbunga hicho kinatarajiwa kutua nchini Msumbiji, katika eneo kitakapotua na mpaka wa Tanzania kuna umbali wa kilomita 230, na athari zake zinatarajiwa kukumba maeneo yaliyo ndani ya kilomita 600.

Kwa mujibu wa taarifa ya TMA, Kimbunga Kenneth kitakuwa ni kimbunga cha pili kuwahi kuikumba Tanzania (cha kwanza kwa ukubwa na athari), ambapo cha kwanza kilitokea mwaka 1952 na kufika katika maeneo ya mkoa wa Lindi.

Kimbunga hicho (cha 1952) hakikuwa na madhara makubwa kutokana na uchache wa watu kipindi hicho, na miundombinu haikuwa imeendelezwa kama ilivyo sasa.

Share.

About Author

Leave A Reply