Friday, August 23

Kilimo kinatoa usalama wa chakula kwa asilimia 100 Tanzania- Rais Magufuli

0


Rais Dkt Magufuli amepongeza utaratibu wa kuwa na siku rasmi ya ufunguzi wa msimu wa soko la tumbaku na kubainisha kuwa zao hilo sio tu lina umuhimu mkubwa nchini Malawi bali pia nchini Tanzania.

Rais Magufuli ameyasema hayo mapema leo alipokuwa nchini Malawi ambapo yeye na Rais wa Malawi, Prof. Arthur Peter Mutharika walipotembelea mnada wa tumbaku wa Lilongwe uliopo Kanengo.

Alisema nchini Tanzania zao la Tumbaku limekuwa miongoni mwa mazao yanayochangia fedha nyingi za kigeni ambapo katika kipindi cha miaka 5 iliyopita limechangia Dola za Marekani Bilioni 1.333 (sawa na shilingi Trilioni 3 na Bilioni 270).

Ameongeza kuwa licha ya kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi za Afrika, sekta hii imeendelea kukabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo teknolojia duni, ukosefu wa pembejeo na elimu duni ya ugani na hivyo ametoa wito kwa viongozi na wadau wote wa kilimo kufanyia kazi changamoto hizo na kulinda maslahi ya wakulima.

Nchini Tanzania sekta ya kilimo inatoa usalama wa chakula kwa asilimia 100, inatoa ajira kwa asilimia 70, inatupatia asilimia 60 ya malighafi za viwandani, inachangia asilimia 30 ya Pato la Taifa na inatupatia fedha za kigeni kwa asilimia 25, hii yote inathibitisha kuwa kilimo ni sekta nyeti na muhimu sana Barani Afrika, amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli ametoa wito kwa viongozi wa nchi za Afrika kuongeza mkazo katika ujenzi wa viwanda utakaosaidia kuongeza thamani ya mazao ya kilimo yanayozalishwa na wakulima na hivyo kuwaongezea kipato.

Tumbaku
ni zao kuu la biashara nchini Malawi ambalo kwa msimu uliopita liliingizia Dola
za Marekani Milioni 300 (sawa na
shilingi Bilioni 713
).

Share.

About Author

Leave A Reply