Thursday, August 22

Kauli ya kwanza ya Waziri Kigwangalla baada ya Rais kuiongezea muda Bodi ya Utalii

0


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amezungumzia hatua ya Rais Dkt Magufuli kuiongezea muda bodi ambayo alitangaza (waziri) kuivuanja mapema Januari mwaka huu.

Januari 18 mwaka huu akizungumza na waandishi wa habari, Dk Kigwangalla alitangaza kuivunja Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu ya utalii, na hivyo kusababisha yeye kutukanwa.

Baada ya tangazo hilo, jana Aprili 23, Rais Dk Magufuli alitangaza kuiongezea muda wa miaka mitatu bodi hiyo, hadi Aprili 23, 2022.

Kufuatia hatua hiyo watu wengi waliona kuwa Waziri Dk Kigwangalla hakuna na mamlaka ya kutengua kauli bodi, ndiyo sababu iliendelea kuwepo licha ya agizo lake.

Hata hivyo waziri huyo amesema kuwa haoni shida kurekebishwa na kiongozi aliyempa uwaziri, kwani ndio anajifunza na wala kukosea sio shida.

Hata hivyo kama nilikosea kwani kuna ubaya nikirekebishwa na Rais wangu aliyenipa uwaziri?! Mbona siyo issue kabisa?! alisema waziri huyo.

Waziri Kigwangalla ambaye amekuwa katika wizara kwa miaka minne, amesema haoni shida kujifunza kwa mtu ambaye amekuwa katika wizara tofauti kwa miaka 20.

Rais alikuwa Waziri kwa miaka 20, mimi ndiyo kwanza mwaka wa nne…bado najifunza! Acha Rais anifundishe, siyo kosa kukosea! Na sioni aibu kufundishwa na gwiji.

Share.

About Author

Leave A Reply