Friday, August 23

Jinsi ya kufahamu spidi tairi ya gari inaweza kwenda na mzigo inaoweza kubeba

0


Hivi umepata kufikiri hata mara moja toka umeanza kumiliki/kuendesha gari ni mambo gani yanakuhakikishia usalama wako? Kwa hakika yapo mengi mfano, ustadi wako wa udereva na umakini uwapo barabarani, uzima wa chombo unachokiendesha kuanzia kwenye injini hadi kwenye matairi pamoja na kufuata kikamilifu kanuni, taratibu na sheria na alama za barabarani.

Je unafahamu nini kuhusu uzima wa matairi ya gari lako? Je unajua kwamba matairi ya gari lako yanayo taarifa muhimu juu ya mwendo gani yanaweza kumudu na ubebe mzigo kiasi gani? Je unajua kwamba ukikimbiza gari lako kwa mwendo ambao ni mkubwa kuliko tairi lako linavyoweza kuhimili au ukibeba mzigo mkubwa kuliko uwezo wa matairi yako unaweza kusababisha yapasuke na kukuletea ajali mbaya na pengine kukusababishi kifo chako, cha uwapendao na hata ulemavu wa kudumu?

Kwenye tairi lolote la gari kuna namba na maandishi mbali mbali. Maandishi yanabeba majina ya aina ya hayo matari kama vile YANA, GENERAL TYRE, APPOLLO, BRIDGESTONE n.k.

Namba zipo zinaonesha tairi imetengenezwa wiki ya ngapi ya waka gani, na inaweza kutumika bila kuleta madhari hadi mwaka gani. Hizi sizo ninazotaka kuzizungumzia leo.

Namba zinazoonekana katika mfumo huu 215/55/R16 91 V. 215 zinawakilisha upana wa tairi. Namba 55 inawakilisha urefu wa tairi kutoka inapokanyagia hadi kuikuta rim, namba 16 inamaanisha saizi ya rim inayoweza kuvalishwa tairi hii.

Namba zinazofuata yaani 91 V ndio ninazozikusudia kuzieleza leo. Namba 91 ipo hapa kwa mfano, inaweza ikawa namba yoyote kulingana na tairi husika imekusudiwa ifanye nini. Hii inawakilisha uzito ambao gari iliyofungwa tairi hiyo inaweza kuhimili.

Herufi “V” na yenyewe ipo hapa kwa mfano na inaweza ikawa herufi yeyote kama vile “H”, “L”, “M”, “N” “O” “P” “Q” “R” “S” “T” “U” “V” “W” “Y”“W”. Herufi hizi zinawakilisha mwendokasi unaoruhusiwa na matairi haya. Na ili uweze kuzielewa zipo orodha ya namba na herufi ambazo zinatambulika kimataifa kama tafsiri sahihi ya mafumbo-namba haya.

Tuanze na mafumbo ya mzigo kiasi gani unaruhusiwa wa tairi yako;
62…… inaruhusiwa kubeba hadi Kg 265
75…… inaruhusiwa kubeba hadi Kg 387
88……. inaruhusiwa kubeba hadi Kg 560
101…… inaruhusiwa kubeba hadi Kg 825
114……. inaruhusiwa kubeba hadi Kg 1180
63….. inaruhusiwa kubeba hadi Kg 272
76….. inaruhusiwa kubeba hadi Kg 400
89…. inaruhusiwa kubeba hadi Kg 580
102…. inaruhusiwa kubeba hadi Kg 850
115…. inaruhusiwa kubeba hadi Kg 1215
64……. inaruhusiwa kubeba hadi Kg 280
77……. inaruhusiwa kubeba hadi Kg 412
90……. inaruhusiwa kubeba hadi Kg 600
103…… inaruhusiwa kubeba hadi Kg 875

Angalia nyingine kwenye intaneti https://www.ctyres.co.uk/general/load-index

Hivyo kama gari yako ina namba 62 ambayo inaruhusu kubeba hadi kg 265 tu huwezi kubeba mzigo wenye uzito wa Kg 387 ambao tairi yenye nambari 75 ndiyo inayomudu au yenye nambari ya juu Zaidi.

Mafumbo namba ya mwendokasi na maana yake ni kama yafuatayo:
L…..inaruhusu hadi 120 Km/h.
M…..inaruhusu hadi 130 Km/h
N…..inaruhusu hadi 140 Km/h
P…..inaruhusu hadi 150 Km/h
Q…..inaruhusu hadi 160 Km/h
R…..inaruhusu hadi 170 Km/h
S…..inaruhusu hadi 180 Km/h
T…..inaruhusu hadi 190 Km/h
U…..inaruhusu hadi 200 Km/h
H…..inaruhusu hadi 210 Km/h
V…..inaruhusu hadi 240 Km/h
W…..inaruhusu hadi 270 Km/h
Y…..inaruhusu hadi 300 Km/h

Angalia mafumbo namba nyinginezo kwenye internet http://www.tirerack.com/tires/tiretech/techpage.jsp…

Hivyo ikiwa tairi yako ina namba L inayokuruhusu spidi hadi 120 na si zaidi, jua hauwezi kuendesha kwa spidi 150 ambayo ni kwa ajili ya nambari “P” au ya zaidi yake.

Unaweza kumshirikisha mwingine taarifa hii muhimu, ili kila mmoja afahamu kwa usalama wake na wengine.

Chanzo: RSA

Share.

About Author

Leave A Reply