Sunday, August 25

Faida 10 zitokanazo na kuwa na Kitambulisho cha Taifa

0


Kwa mujibu wa Rais Dkt Magufuli, hadi sasa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) tayari imetoa vitambulisho hivyo kwa wananchi milioni 13 au 15, kati ya wananchi takribani milioni 55.

Rais aliyasema hayo juma lililopita akiwa mkoani Mbeya ambapo bado anaendelea na ziara yake ya kikazi alipokuwa akizungumzia suala la usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole lililotangazwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na kampuni za mawasiliano.

Ili kuweza kusajili laini ya simu, TCRA na kampuni hizo zimeeleza kuwa kila mwananchi atatakiwa kutumia kitambulisho cha taifa katika usajili.

Tanzania ina watu milioni 55, na vitambulisho vya Taifa vimetolewa ni watu milioni 13 au 14. Sasa unaposema watu wasajili laini kwa kutumia vitambulisho vya Taifa, wakati NIDA haijatoa vitambulisho vya Taifa kwa wote, ina maana unataka Watanzania wasitumie simu,? alihoji Rais Magufuli

Kufuatia kauli hiyo, aliagiza zoezi la usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole liende hadi Disemba, ili kila mmoja awe amepata kitambulisho hicho.

Lakini mbali na kusaidia katika usajili wa simu au usajili mwingine wowote ule, vitambulisho vina faida lukuki.

Hapa chini ni faida zinazoweza kupatikana kutokana na kuwa na kitambulisho cha taifa:

  1. Vitasaidia kuongeza wigo wa mapato ya Serikali
  2. Vitasaidia kumtambua mhusika kirahisi anapohitaji kupatiwa huduma katika taasisi mbalimbali kama vile benki, taasisi za mikopo na huduma za afya.
  3. Vitarahisisha kuwatambua wakwepaji wa kurejesha mikopo kutoka kwenye benki na asasi mbalimbali za fedha nchini.
  4. Vitasaidia kuweka kumbukumbu za matukio ya uhalifu katika daftari la kumbukumbu la kielektroniki.
  5. Vitawezesha kumtambua mtu anapofanya biashara au shughuli nyengine kwa kutumia majina tofauti.
  6. Vitafanikisha kuhakikisha kuwa mtu anapata stahili zake za jamii. Kwa mfano, kupata malipo ya pensheni, haki za matibabu, haki za kujiunga na masomo ikiwa ni pamoja na stahili zozote ambazo raia wa Tanzania anastahili kupata kirahisi kwani kupitia kitambulisho mtu atatambulika kirahisi(nani ni nani?, yuko wapi?, na anafanya nini? katika taifa hili.
  7. Vitasaidia  kuondoa watumishi hewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara ‘payroll’ ya Serikali.
  8. Vitaimarisha utendaji kazi Serikalini kwa kuwa na kumbukumbu sahihi za watumishi na malipo ya stahili zao, hasa pale wanapostahafu.
  9. Vitarahisisha zoezi la kuhesabu watu (sensa).
  10. Vitarahisisha zoezi la kuhuisha daftari la wapiga kura, ambapo kwa sasa hufanyika mara mbili kabla ya uchaguzi mkuu.

Mbali na kutuoa vitambulisho vya taifa, NIDA pia hutoa vitambulisho vya wakimbizi na vitambulisho vya wageni wakazi.

Share.

About Author

Leave A Reply