Sunday, August 18

Fahamu makundi mbalimbali ya alama za barabarani na maana zake

0


Mshirikishe mwenzako:

MAENDELEO ya kiuchumi duniani yanaenda sambamba na uimara wa miundombinu hasa ya barabara jambo ambalo ni kichocheo kikubwa cha kuleta mabadiliko na kujua ni kwa namna gani uchumi wa dunia umekua.

Miundombinu ya barabara kwa baadhi ya maeneo hasa hapa nchini kwetu imekuwa na changamoto kadha wa kadha ambapo wakati mwingine imekuwa ikizorotesha ukuaji wa kimaendeleo kwa baadhi ya maeneo na kuyafanya kutokufikika kwa urahisi.

Licha ya serikali kujitahidi katika kuboresha miundombinu ya barabara lakini zipo changamoto zinazosababishwa na watumiaji wa miundombinu hiyo ya barabara ambapo kwa kiasi kikubwa huchangiwa na uzembe wa binadamu kwa kutotii sheria, alama na michoro ya barabarani jambo ambalo limekuwa likichangia kutokea kwa ajali nyingi ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya watu na mali zao.

Wengi wamepoteza maisha na taifa kupoteza nguvu kazi na pia wengine wamebakia na ulemavu wa kudumu kiasi cha kushindwa kujitafutia kipato cha kila siku na kuwa mzigo kwa familia zao ama wategemezi wao na kuiacha familia anayoipenda kuishi maisha yasiyo na dira.

Wapo baadhi ya madereva wa magari ambao hujitahidi kuzingatia sheria, alama na michoro ya barabarani lakini yapo matatizo yanayosababishwa ama kuchangiwa na baadhi ya wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara kwa kung’oa alama za barabarani ambazo zinamuelekeza dereva wa chombo cha moto kwa kumpa tahadhari ya mbele anapokwenda lakini alama hii haiwezi kuonekana na matokeo yake husababisha ajali kutokea na kuyagharimu maisha ya watu.

Hapa chini ni alama za barabarani ambazo dereva na mwendeshaji yeyote wa chombo cha moto anapaswa kuzifahamu na kuzizingatia anapoendesha chombo cha moto, ili kuhakikisha uasalama wake, wa wengine, pamoja na mali zao.

Facebook Comments
Share. Twitter Facebook Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr Email

About Author

Leave A Reply