Sunday, August 18

Diamond na Zari warushiana maneno kisa kuchepuka

0


Nyota wa muziki nchini Tanzania, Naseeb Abdul maarufu kwa jina la sanaa, Diamond Platinumz amedai kwamba mzazi mwenzake hakuwa mwaminifu katika uhusiano wao na ndio sababu kubwa iliyopelekea wawili hao kuachana.

Akizungumza katika kipindi cha Block 88. Diamond alisema kuwa Zarinah Hassan, maarufu Zari alikuwa na uhusiano wa kando (alikuwa anachepuka) na msanii mmoja wa Nigeria.

Diamond na Zari ambaye ni mfanyabiashara wa Uganda anayeishi Afrika Kusini wamezaa watoto wawili, Tiffah na Abdul ambao wote wanaishi na mazazi wao wa kike Afrika Kusini.

Hata hivyo Zari ambaye amekuwa na uhusiano na Diamond kwa miaka mitatu amekanusha shutuma hizo zilizoelekezwa kwake.

Diamond aliendelea kuporomosha shutuma nzito kwa Zari akidai mama wawili huyo alikataa kuhamia Tanzania ili waweze kuwa pamoja.

Kama kijana mdogo ambaye ni nyota na nina hisia nyingi , haiwezakani kwamba ningesubiri zaidi ya miezi mitatu bila kushiriki tendo la ngono.Nilikuwa tayari kumuanzishia Zari biashara nchini Tanzania , lakini akakataa kuondoka Afrika Kusini. Mulikuwa munatarajia nifanye nini? alihoji Diamond.

Hata hivyo Diamond alimsifia Zari akisema kuwa alikuwa ni mwanamke mwenye sifa za kuwa mke na kwamba alimpenda sana. Pia alizingumzia tuhuma zilizowahi kutolewa na Zari kwamba kunawakati hakutuma fedha za matumizi ya watoto, ambapo amesema ni kweli hakutuma sababu mzazi huyo wa kike alimzuia kuzungumza na wanae.

Kwa sasa Diamond ana uhusiano na staa kutoka Kenya, Tanasha Oketch, wakati kwa upande wa Zari karibuni alimtambulisha mpenzi wake lakini hakuonesha sura yake, huku akimmwagia sifa mbalimbali, na kwamba yeye ni mwanaume aliyetoka mbinguni kwani ameweza kumpenda yeye licha ya kuwa na umri mkubwa na watoto watano.

Share.

About Author

Leave A Reply