Sunday, August 18

SportPesa kukarabati Nyumba ya Daktari Zanzibar

0


Kampuni nguli ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa Limited, imekubali kufanya ujenzi wa nyumba kwa ajili ya daktari katika eneo la Kizimkazi, mkoa wa Kusini Unguja.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti kutoka SportPesa Tanzania, Bwana Tarimba Abbas amesema “Ikiwa bado tuko mwanzoni mwa mwaka 2018 kampuni yetu tumeamua kutoa mchango wetu kwa jamii ya Zanzibar kwa kumalizia ujenzi wa nyumba ya madaktari ambayo ujenzi wa awali ulifanyika miaka 30 iliyopita, ujenzi mpya ni pamoja na kuongeza vyumba ili nyumba hiyo iweze kukaliwa na madaktari wengi zaidi.

“Kwa wanazanzibari wote, sisi kama SportPesa tupo kwa ajili yenu na si kwa uoande wa bara tu na ndiyo maana tumeamua kukarabati makazi ya madaktari kwani wapo kwa ajili ya kuokoa maisha yetu na ya watu wanaotuzunguka.

“Ujenzi wa nyumba hizi itaanza haraka iwezekanavyo na itachukua si zaidi ya kipindi cha miezi sita hadi kukamilika.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa nyumba hiyo, Diwani wa Wadi ya muyuni Bwana Mustafa Mohammed Haji alianza kwa kuwakaribisha wawakilishi kutoka SportPesa kwenye wilaya yake na Zanzibar.

“Napenda kuipongeza kampuni yenu kwa kazi nzuri mnayoifanya ikiwa pamoja na mambo mbalimbali mnayofanya ili kuendeleza na kukuza sekta ya michezo nchini”

“Nilipopata taarifa juu ya ujio wenu kiukweli nilifarijika sana maana nawaamini na nategemea mambo mazuri kutoka kwenu kwani kwa mara ya kwanza kusikia SportPesa ni kipindi kile mlivyoichukua timu yetu ya mpira wa miguu Jang’ombe kushiriki mashindano ya SportPesa SuperCup mwaka jana”

Huu utakuwa ni muendelezo wa huduma za kijamii ambazo kampuni ya SportPesa imeendelea kuchangia ili kubadili maisha ya watanzania katika nyanja mbalimbali za kimaisha.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.