Sunday, August 18

Kikosi cha Taifa Stars kinachoanza dhidi ya Algeria aleo usiku

0


Taifa Stars

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza kikosi cha mwisho kitakachoanza dhidi ya wenyeji Algeria katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika leo saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki Uwanja wa 5 July jijini Algiers.

Katika kikosi hicho, Kocha Mayanga amewaanzisha nahodha Mbawana Samatta sambamba na Saimon Msuva na Shiza Kichuya katika eneo la ushambuliaji, huku Himid Mao, Mudathir Yahya na Said Ndemla wakipewa jukumu la eneo la kiungo cha ulinzi na uchezaji.

Walinzi Kelvin Yondani, Abdi Banda watasaidiwa na Shoamari Kapombe na Gadiel Mbaga katika kuhakikisha milingoti ya Aishi Manula inakua salama muda wote wa mchezo.

Kikosi kamili cha Taifa Stars kinachoanza dhidi ya Algeria:

GK – Aishi Manula,

Shomari Kapombe, Gadiel Mbaga, Abdi Banda, Kelvin Yondani –

Himid Mao, Mudathir Yahya, Said Ndemla –

Mbwana Samatta, Saimon Msuva, Shiza Kichuya

Wachezaji wa Akiba:

GK Ramadhan Kabwili, GK Mohamed Abdulrahman, Hassan Kessy, Erasto Nyoni, Abdoulaziz Makame, Mohamed Issa, Ibrahim Ajibu, Feisal Salum, Yahyza Zayd, ‘Shaban Chilunda na Rashind MandawaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.