Tuesday, August 20

Baadhi ya wachezaji waliocheza timu moja hadi kustaafu

0


Rogerio Cen

Huyu alikuwa mlinda mlango wa Brazil na Sao Paulo akiichezea mechi 1238 bila kuhama mpaka kustaafu kwake .

Rogerio yupo katika kumbukumbu za kitabu cha Guiness kama mchezaji aliyecheza mechi nyingi kwa timu moja bila kuhama mpaka kustaafu. A-One-club man.

Francesco Totti

Huyu alipata kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Italia. Pia ni mmoja wa wachezaji waliocheza timu mmoja kwa mechi nyingi mpaka kustaafu. Totti alijiunga na klabu ya Roma mwaka 1992 mpaka mwaka 2017 alipoamua kustaafu akiwa amechez mechi 619 na kufunga magoli 250.

Paolo Maldin

Huyu ni gwiji wa klabu ya AC Milani aliyojiunga nayo mwaka 1985 hadi mwaka 2009 alipostaafu soka. Maldini ameichezea Milani mechi 647 akitupia nyavuni goli 29 tu katika misimu 25 ya Seria A. Kwa ujumla amecheza mechi 902 kwa klabu yake na timu ya taifa akishikiria rekodi ya muda mrefu ya unahodha Milani na timu ya taifa ya taifa ya Italia.

Jamie Caragher

Hili ni gwiji la soka viunga vya Jiji la Liverpool . Alijiunga na klabu hiyo mwaka 1996 mpaka mwaka 2013 alipoamua kustaafu soka. Alipata kuichezea klabu hiyo mechi 737 katika misimu 16 bila ubingwa wa ligi kuu ya England. Ni moja ya walinzi bora kuwahi kutokea katika klabu ya Liverpool.

Ryan Joseph Giggs

Huyu ni mmoja wa viungo bora kuwahi kuichezea klabu ya Manchester United akijiunga nayo mwaka 1990 hadi mwaka 2014 alipoamua kuachana na soka. Alipata kuichezea klabu hiyo zaidi ya mechi 900+ katika michuano yote.

By Samuel SamuelRead More

Share.

About Author

Comments are closed.