Sunday, August 25

Ndani ya siku 40 Samsung wauza Galaxy A milioni 2!

0


vodacom swahili

Kampuni ya Korea Kusini ya Samsung imeuza simu zake za Familia ya Galaxy A takribani milioni mbili ndani ya siku 40 katika nchi ya India.

Mauzo ya simu hizo yalianza mwezi Machi tarehe 1 na kupata mapato ya $500 milioni ambapo malengo ya kampuni hiyo ni kupata $4 bilioni kwa mwaka kutokana na mauzo ya Simu za galaxy A.

Siku 40

Muonekano wa simu za Samsung Galaxy A

Mapema mwezi huu Samsung ilitangaza kuzindua simu ya Galaxy A20, ikiwa ni simu ya nne katika mfululizo wa simu za Galaxy A. Mwezi Machi Samsung ilizindua Galaxy A10 (Tsh. 280,000), Galaxy A30 (Tsh. 565,000) na Galaxy 50 (Tsh. 758,500).

Kupitia Afisa mkuu wa Masoko na Makamu wa rais wa Samsung India, Bw. Ranjivjit Singh alisema wamepata dola za Marekani 500 milioni baada ya kuuza aina tatu za Galaxy kwa siku 40 tu. Aliongeza kusema kwamba hiyo inaweza kuwa ni rekodi ya mauzo kwa simu hizo nchini India.

Mpango wa Samsung India ni kuendelea kuzindua simu za Galaxy A kwa kila mwezi kuanzia Machi mpaka Juni mwaka 2019. Mwezi Mei 2019 Samsung wanatarajia kuzindua Galaxy A80; Galaxy A70tayari imeshazinduliwa nchini India.

Share.

About Author

Leave A Reply