Thursday, August 22

Mwanamume aliyejibadilisha jinsia 'Mmnyonyesha mtoto'

0


Mtoto ananyonyaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mwanamume aliyejibadilisha jinsia na kuwa mwanamke amefanikiwa kumnyonyesha mtoto katika kisa cha kwanza cha aina yake kuwahi kushuhudiwa, watafiti wanasema.
Mwanmke huyo mwenye umri wa miaka 30 alitaka kumnyonyesha mtoto baada ya mpenzi wake aliyejifungua kusema hataki kumnyonyesha mtoto huyo, hayoni kwa mujibu wa wa jarida la afya la watu waliojibadili jinsia.
Alifanikiwa kunyonyesha baada ya kumeza dawa na kukamua maziwa, ripotihiyo inasema kutoka nchini Marekani.
Mtaalamu wa Marekani anasema utafiti huo huenda ukachangia visa zaidi vya wanaume walijibadilisha jinsia kuwa wanawake kunyonyesha watoto.
Mwanamke huyo aliyekuwa anapokea matibabu ya kubadili homoni zake mwilini kwa muda wa miaka 6, lakini hajafanyiwa upasuaji kubadili sehemu zake za siri, wakati alipowaomba madaktari wamsaidie atimize lengo lake la kumnyonyesha mtoto.
Kabla ya mtoto huyo kuzaliwa, madakatari walimpadawa za miezi mitatu unusu kumsaidia kupata maziwa, kwa kawaida dawa hizo hupewa wanawake waliowaasili watoto au waliojipatia watoto kupitia wanawake wanobeba mimba kibiashara kuwaisaidia wasioweza kuzaa.
Dawa hizo husisimua homoni mwilini kushinikiza kutoa maziwa na kuzuia homoni za kiume na pia alihitajika kukamua maziwa yake.
Na mtokeo yake, yalimsababisha mwanamke huyo kuweza kupata maziwa kiasi.
Watafiti wanasema mtoto huyo alikunywa maziwa hayo tuu kwa wiki zake sita za uhai, wakatiambapo ukuwaji wake, ulaji na uwendaji haja wake ulikuwa unaendelea kama kawaida.
Baada ya hapa, mtoto alianza kupewa maziwa ya mkebe kwasababu maziwa yalianza kupungua.
Mtoto huyo sasa ana miezi sita na anendelea kunyonya kama sehemu ya lishe yake, wahiriri wa utafiti huo wanasema.
Watafiti wamesema utafiti zaidi unahitajika kubaini matibabu halisi ya wanaume wanaojibadili jinsia kuwa wanawake wanaotaka kunyonyeshaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatafiti wamesema utafiti zaidi unahitajika kubaini matibabu halisi ya wanaume wanaojibadili jinsia kuwa wanawake wanaotaka kunyonyesha
Dkt Channa Jayasena, mhadhiri mkuu katika chuo cha Imperial College anayejishughulisha na masuala ya uzazi amesema, utafiti huo ni ‘hatua nzuri’.
Amesema ameshasikia visa kadhaa nchini Uingereza vya wanaume waliogeuka kuwa wanawake wanasaidiwa kunyonyesha, lakini mpaka sasa hakuna ripoti iliyochapishwa.
Amesema:”Tunachohiaji kufanya nikuvikusanya visa hivi na tusaidiane ki mawazo, tutafute mbinu muafaka kuwasaidia kunyonyesha bila ya kuwadhuru ki afya.”
Watafiti wanasema haijabainika wazi iwapo dawa zote zinzotumika zinahitajika kufanikisha wazazi hao kuwawezesha kunyonyesha.
Wamesema uchunguzi zaidi unahitajika kubaini matibabu halisi ya wanaume wanaojibadili jinsia kuwa wanawake wanaotaka kunyonyesha.

Mada zinazohusianaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.