Tuesday, August 20

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU 'RAIS' JACOB ZUMA

01. Jina lake kamili ni Jacob Gedleyihlekisa Zuma. Jina Gedleyihlekisa maana yake anacheka huku akisaga adui zake. Jina la ukoo wake ni Msholozi. Yeye alizaliwa tarehe 12 Aprili 1942 huko Nkandla, KwaZulu-Natal.
2. Jacob Zuma hakuwa na elimu rasmi tangu akiwa mtoto. Baba yake alikua polisi, alifariki mwishoni mwa vita kuu ya pili ya dunia wakati huo Zuma akiwa na umri wa miaka mitano. Baada ya kifo cha baba yake, mama yake alipata kazi kama mfanyakazi wa nyumbani (House girl). Hivyo Zuma hakua na elimu rasmi ya kumwezesha kumsaidia mama yake. Alijifundisha mwenyewe kusoma na kuandika Kizulu katika kichaka. Pamoja na kua na hali hiyo haikumkatisha tamaa kuacha kujifunza lugha nyingine. Zaidi ya Zulu, yeye anaongea Kifaransa, Kirusi, Kireno Kiswahili na Xhosa kwa ufasaha.
3. Jacob Zuma alipata mafunzo kutoka Umoja wa Kisovieti (USSR). Alianza kujihusisha katika siasa akiwa na umri wa miaka 17 wakati alipojiunga na ANC. Akawa mshiriki wa Umkhonto We Sizwe, na kiongozi wa wanamgambo wa ANC, mwaka 1962. Hii ilikuwa baada ya serikali ya Afrika Kusini kupiga marufuku chama. Alijiunga na chama cha kikomunisti cha Afrika Kusini (SACP) mwaka 1963. Wakati akiwa mwanachama wa chama cha kikomunisti ndipo alipata mafunzo ya kijeshi katika Umoja wa Kisovieti. Baadaye alijiunga na ANC Idara ya upelelezi ambapo alikuwa mkuu wa upelelezi.
4. Alifungwa gerezani katika kisiwa cha Robben kwa miaka 10. Mwaka 1963, Zuma alikamatwa pamoja na askari 45 wa ANC. Walitiwa hatiani kwa kula njama ya kuipindua serikali ya ubaguzi wa rangi na hivyo walihukumiwa kutumikia kifungo katika kisiwa cha Robben pamoja na Nelson Mandela na viongozi wengine maarufu wa ANC. Wakati akiwa katika kisiwa cha Robben, alihudumu kama mwamuzi wa timu ya mpira ya wafungwa, michezo ambayo ilitayarishwa na uongozi wa wafungw, Makana F.A.
5. Mwaka 1987, Jacob Zuma Alilazimishwa kuondoka Msumbiji. Serikali ya Msumbiji ilimuamuru Zuma kuondoka nchini humo. Aliondoka Msumbiji kupitia Lusaka, kwenda Zimbabwe. Wakati huo Makao makuu ya ANC yalikua yamehamia nchini Zimbabwe na aliteuliwa kuwa mkuu wa miundo ya ardhini.
6. Zuma alikumbwa na madai ya ufisadi na ubakaji. Mwaka 1999, wakati alipokuwa Makamu wa Rais wa Afrika ya Kusini, alipata mashtaka ya rushwa kwa ajili ya matumizi mabaya ya randi milioni 29 ambazo alisema zilitumika kwa ajili ya kununua silaha za kimkakati kama vile ndege, boti, submarines na helikopta. Mashtaka yalifutwa baadaye mwaka 2003. Hata hivyo aliingia katika tuhuma tena baada ya Mshauri wake wa fedha kutiwa hatiani kwa rushwa na udanganyifu. Matokeo yake, Thabo Mbeki, aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, alimfukuza kazi Zuma kutoka nafasi yake kama makamu wa Rais.
Jacob Zuma wakati fulani alikabiliwa na mashtaka ya ubakaji mwaka 2005 baada ya mwanamke aliedai kumbaka nyumbani kwake. Ni wakati huu ambapo alipata wakosoaji wengi kulingana na kutojua kwake hatari ya kufanya ngono na mwanamke huyo bila kutumia kinga jambo ambalo alijitetea kua baada ya tendo la ngono aliwahi bafuni kuoga hivyo haikua rahisi kwake kuambukizwa UKIMWI. Hatimaye hakimu alimfutia mashitaka zuma ikiwemo yale ya rushwa.
7. Zuma ana wake wanne na watoto 21. Amekuwa na ndoa ya wake sita, lakini mpaka sasa ana ndoa na wanawake wanne kwani mmoja wa wanandoa wake alikufa, na mwingine kutalikiana. Mwaka 2003, alilipa mahari ya ng’ombe 10 kuomba mkono aoe katika familia ya Malkia Sebentile Dlamin wa Swaziland. Huyu alipaswa kua mke wa tano lakini familia ya kifalme ya Swaziland iliingia kinyongo kwa sababu yeye kamwe hakufanya maandalizi yeyeoye ya sherehe ya kuoa japo alikua amelipa mahali yote.
8. Jina lake kisiasa lilkuja juu wakati hali ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi ilikua juu nchini Afrika ya Kusini. Wakati huo ilikadiriwa watu milioni 6 walikua wagonjwa wa UKIMWI nchini Afrika Kusini. Hata hivyo, mipango ya Jacob Zuma kuboresha huduma ya afya, hasa kwa wagonjwa wa UKIMWI ilisababisha kuboresha afya na kuishi kwa muda mrefu zaidi kuliko miaka kabla (miaka 60).
9. Zuma aliporomoka kisiasa wakati alipofukuzwa kama makamu wa Rais mwaka 2005. Thabo Mbeki, alimfukuza kazi Jacob Zuma kutoka nafasi yake kama makamu wa Rais kutokana na tuhuma dhidi yake juu ya ulaghai na rushwa. Alipelekwa mahakamani, lakini mashtaka dhidi yake yalifutwa kufuatia mwenendo wa mashitaka.
10. Zuma anatambulika kama mtu wa watu. Zuma anajulikana kuwa na utu, ana historia ya mandhari ya Afrika ya kusini. Ana historia ya unyenyekevu na kufanya kazi isiyo ya kawaida ili kusaidia familia yake hususan baada ya baba yake kufariki. Hata hivyo, yeye amepata mafanikio makubwa. Hadithi yake, kwa hiyo, inaonyesha matumaini kwamba hali uliyokua nayo huko ulikotoka haimaanishi uhalisia wa huko uendako.

LikeShow more reactions

CommentRead More

Share.

About Author

Comments are closed.