Thursday, August 22

KIVITA, MKOMBOZI WA WAKULIMA TANZANIA YAANZISHWA

0


 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (kushito), akizungumza katika kikao cha pamoja  na Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema) cha kujadili uanzishwaji wa Taasisi ya Kilimo, Viwanda Tanzania (KIVITA), Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mratibu wa Washona Mahema, Azory Lugamba, Ofisa Mtendaji Mkuu Msaidizi wa Washona Mahema, Ulimbumi Korosso, Mwenyekiti wa Washona Mahema, Shadrack Chilongani na Mkurugenzi Mtendaji wa Washona Mahema, Askofu, Edger Mwamfupe.

Na Richard Mwaikenda, Mnazi Mmoja
TAASISI mpya ya Kilimo Viwanda Tanzania (KIVITA), imeundwa kwa lengo la kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wananchi kuhusu maendeleo ya Kilimo Biashara na Viwanda.

Kivita imeanzishwa kwa ushirikiano wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) na Taasisi ya Hope For All (Washona Mahema).

Taasisi hizo mbili ambazo karibu malengo yao yanafanana zimeamua kuuanda Kivita ili kutimiza ndoto ya kuwaendeleza wananchi kwa njia ya mafunzo ili wazalishe mazao yenye ubora ili kutosheleza soko la ndani na nje ya nchi.

Pia wazalishe mazao ambayo tayari yana soko la uhakika hivyo kuondokana na hasara walioyokuwa wanaipata awali kwa kuzalisha mazao bila kujua soko liko wapi.

Pia, Kivita itasaidia jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kuendeleza viwanda nchini, kwa kuwaelekeza wananchi kuzalisha mazao yatakayokidhi mahitaji ya malighafi ya viwanda vitakavyojengwa nchini.

Mkikita na Washona Mahema ambao kwa ujumla hivi sasa wana zaidi ya wanachama 12,000 nchini, wana mipango ya kutoa mafunzo ya kuwabadilisha kifikra watanzania kutoka kwenye kilimo cha kutumia jembe la mkono na kuwapeleka kwenye kilimo cha kutumia zana za kisasa chenye mafanikio makubwa.

 Kivita itawatumia wataalamu waliobobea katika masuala ya kilimo na ufugaji pamoja na masoko kutoka Mkikita na Washona Mahema. Wataandaa makongamano kuanzia vijijini, wilayani na mikoani. 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202,0689425467,0754264203


 Wakiendelea na kikao hicho. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Mkikita, Deo Liganga na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mkikita, Elizabeth Ndamgoba.

  Ofisa Mtendaji Mkuu Msaidizi wa Washona Mahema, Ulimbumi Korosso,

 Mwenyekiti wa Washona Mahema, Shadrack Chilongani 

  Mratibu wa Washona Mahema, Azory Lugamba

 Mkurugenzi Mtendaji wa Washona Mahema, Askofu, Edger Mwamfupe.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mkikita, Elizabeth Ndamgoba.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.