Thursday, February 21

MHE. MAHUNDI AKEMEA TABIA ZA USHIRIKINA.

0


 

Mkuu wa wilaya ya Chunya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi leo amefanya ziara katika kata ya Sangambi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.

Akiwa katika kijiji cha Shoga amewaambia wananchi wa kijiji hicho, waepuke imani za kishirikina, haswa tabia inayofanywa na baadhi ya waganga ‘Rambaramba’ ambao wamekuwa wakiwatapeli wananchi na kusababisha chuki miongoni mwao.

Mhe. Mahundi amewaomba wananchi kutowaamini Rambaramba hao, kwani wanasababisha uvunjifu wa amani na kugombanisha jamii kwa ujumla.

“Maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe, hivyo tusiruhusu mtu yeyote kutufarakanisha kwa kisingizio cha kudhibiti uchawi”. amesema Mhe. Mahundi.

Bi. Magnalena Mbega ni mkazi wa Shoga,amesema amekua akiwasikia muda mrefu Rambaramba kuwa ni kiboko ya wachawi.

“Nimezaliwa Chunya hapa na hawa Rambaramba nimekuwa nikiwasikia miaka mingi ingawa sijawai kushuhudia jinsi wanavofanya hizo kazi zao” amesema Bi Magdalena Mbega.

Mhe. Mahundi amewatahadharisha wananchi kuwa makini na kikundi hicho na kuacha kuwa na imani za kishirikina na badala yake waungane katika kujiletea maendeleo.

Rambamba ni kikundi cha waganga wa kienyeji kinachojitangaza kuwa suluhu ya kukomesha wachawi na kimekua kikifanya shughuri hizo maeneo mbalimbali nchini.


Share.

About Author

Leave A Reply