Monday, August 19

“Wanachama wanatakiwa kumpuuza Lipumba”

0


Kamati ya Utendaji ya Taifa ya CUF imetoa maazimio ya kikao cha kawaida kilichofanyika jana Machi 26, 2018 kuhusu masuala mbalimbali ya chama hicho ikiwemo maandalizi ya uchaguzi wa ndani ya chama, hali ya kisiasa nchini, na maendeleo ya kesi zilizoko mahakamani. 

Akizungumza na wanahabari wakati akisoma maazimio ya Kamati hiyo, Katibu Mkuu CUF, Maalim Seif Sharif Hamad  imewaagiza viongozi na wanachama wa CUF ngazi zote kuwafichua na kuwadhibiti watakaogundulika kuwa na nia ya kukihujumu na kukivuruga chama.

“Imeagiza chama kiendelee kufuatilia hujuma hizo kwa lengo la kudhibiti. Imewaagiza viongozi na wanachama wa ngazi zote kuwa makini na kufuatilia hila zote za kukihujumu Chama na kuwafichua wale wote watakaogundulikana kuwa na nia ya kukihujumu Chama. Wanachama wasikubali kuchokozeka, lakini hapo hapo Wanachama waimarishe umoja, mashirikiano na mshikamano, wakitambua kuwa umoja ni silaha mujarabu ya kuwashida maadui wa Chama,” amesema na kuongeza.

“Wanachama wanatakiwa kumpuuza Lipumba, genge lake na propaganda zao za kijinga.
Wanachama wanatakiwa kuwatenga na kutowapa mashirikiano mtu yeyote atakayebainika ni muasi wa Chama anayemuunga mkono Lipumba na genge lake.”

Kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa ndani wa chama hicho, Maalim Seif amesema Kamati imewaagiza viongozi wa CUF katika ngazi za Wilaya, Majimbo, Kata na Matawi pamoja na Wanachama wote kupuuza taarifa iliyotolewa na Prof. Lipumba juu ya Maandalizi ya Uchaguzi wa Chama ndani ya Chama.

“Wanachama wanatanabahishwa kuwa Baraza Kuu Halali la Uongozi la Taifa la CUF lililochaguliwa Juni, 2014 bado halijakaa na kutoa maagizo ya maandalizi ya uchaguzi wa ndani ya Chama. Wala Baraza Kuu haliijatoka agizo lolote kwa Kamati ya Utendaji ya Taifa kuanza jambo lolote linalohusu Maandalizi hayo. Wanachama wanaombwa kuwa wastahamilivu juu ya hili, na wakati utapofika wa Kamati kufanya maamuzi juu Maandalizi ya Uchaguzi wa Chama ndani ya Chama taarifa rasmi itatolewa kwa viongozi wa ngazi zote na wanachama wa kawaida,” amesema.

Kuhusu hali ya kisiasa nchini, amesema Kamati ya Utendaji inaendelea kufuatilia kwa makini malalamiko ya baadhi ya wananchi juu ukiukwaji wa haki za binadamu na kisha kushauriana na wadau wote, ikiwemo Serikali , juu ya kubaini ukweli wa malalamiko hayo, kujua chanzo chake na kuweka mikakati ya kuikomesha hali hiyo. 

Na Regina MkondeRead More

Share.

About Author

Comments are closed.