Sunday, August 18

Ukusanyaji mapato katika jiji la DSM waimarika

0


Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema ukusanyaji kodi katika jiji hilo unakwenda vizuri na kwamba hadi sasa umefikia asilimia 54.

Meya Mwita ameyasema hayo leo baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

“Katika ukusanyaji kodi tunakwenda vizuri, ukusanyaji umefikia 54% hadi kufika mwezi Julai tutakuwa tumevuka lengo,” amesema.

Aidha, amesema Halmashauri ya Jiji inatarajia kufungua masoko mawili katika maeneo ya Tabata na Mbezi ili kuongeza mapato.

Kuhusu maendeleo ya masoko yanayomilikiwa na jiji la Dar es Salaam, ikiwemo la Machinga Complex na Kariako DDC, Meya Mwita amesema kwa sasa yanaendelea vizuri.

Na Regina MkondeRead More

Share.

About Author

Comments are closed.